Home Sports WAWA AFUNGUKIA ISHU YAKE NA PABLO

WAWA AFUNGUKIA ISHU YAKE NA PABLO

PASCAL Wawa, beki wa kati wa Simba, ameweka wazi kuwa hakuna tofauti kati yake na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco.

Juzi, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ilitokea hali ya kutoelewana katika suala la kufanya mabadiliko ambapo Wawa alikuwa anajiandaa kuingia uwanjani akitokea benchi ghafla, Pablo alimvuta kwa nguvu kubwa na kuonekana akilalamika.

Pia Pablo alionekana mwenye hasira ambapo alionekana akipiga kiti na chupa ya maji jambo ambalo liliweza kuonesha kwamba alikuwa amekasirika kwelikweli.

Kutokana na kitendo hicho ilibidi Wawa arudi benchi na kumaliza dakika 90 akishuhudia mchezo huo ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma KMC 1-4 Simba.

Wawa amesema kuwa hakuna tofauti kati yake na kocha wa timu hiyo.

“Hakuna tofauti kati yetu na kocha kila kitu kinakwenda vizuri na tunashukuru kwa kuwa tumeshinda,” alisema Wawa.

Previous articleJEMBE LA SIMBA LAMALIZANA NA TIMU KONGWE
Next articleKIUNGO MBRAZILI KUPEWA MIKOBA YA LWANGA