>

BOSI YANGA ASIMULIA NAMNA AMBAVYO WALIMPA MKATABA SURE BOY

ZAWADI ya Krismasi kwa mashabiki wa Yanga ni saini ya kiungo wa mpira Salum Aboubhakari ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Azam FC.


Jana, Desemba 24 Sure Boy alitambulishwa Yanga kwa dili la miaka miwili ambao dau lake linatajwa kuwa milioni 80
.

Ikumbukwe kwamba Sure Boy alisimamishwa kwenye timu yake ya zamani ambayo ameitumikia kwa muda mrefu Azam FC kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu pamoja na wachezaji wenzake wawili, Mudathiri Yahya na Aggrey Morris.

Tayari Morris na Mudathiri wamerejea kambini na kuendelea na mazoezi lakini Sure yeye aiomba kuvunja mkataba wake jambo ambalo limetimia na sasa yupo zake ndani ya Yanga.

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wamefikia muafaka wa kumsaini nyota huyo baada ya kuisaka saini yake kwa muda mrefu.


“”Ukweli ni kwamba tulikuwa tunahitaji huduma ya Sure Boy kwa muda mrefu na baada ya kuomba kuvunja mkataba hapo ikawa rahisi kwetu kuipata saini yake.

“Tumempa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia Yanga na tunaamini kwamba atafanya vizuri kwani ni moja ya viuongo wenye uwezo mkubwa.

“Napenda pia kuwashukuru Azam FC kwa namna ambavyo wamekuwa ni waungwana hasa katika suala la wachezaji huenda ingekuwa timu nyingine ingetaka kumkomoa mchezaji lakini kwa kuwa imempa ruhusa basi sisi tumeamua kutumia hiyo kuwa fursa,” amesema.