Home Sports REKODI ZA JEMBE JIPYA LA YANGA

REKODI ZA JEMBE JIPYA LA YANGA

REKODI za winga mpya wa Yanga, Chico Ushindi zinatisha jambo ambalo linaonesha ni kweli timuhiyo imepata jembe la maana ambalo litakuja kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inazidi kuwa kiwembe.


Yanga tayari imekamilisha 
usajili wa mkopo wa winga huyo ambaye alikuwa anakipiga katika Klabu ya
TP Mazembe ya nchini DR 
Congo.


Katika mkataba huo, kuna 
kipengele cha nyota huyo anayetumia miguu yote kusakata kabumbu kujiunga
na Yanga moja kwa moja 
kama wataridhika na uwezo wake au kumuuza kisha fedha wagawane na TP Mazembe.

Ushindi ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 25, anamudu vema kucheza nafasi zote za mbele akiwa anacheza winga ya kulia na kushoto, lakini pia anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati namba 9 na wa pili namba 10

Raia huyo wa DR Congo ambaye alijiunga na TP Mazembe msimu wa 2017/18, amefanikiwa kuichezea timu hiyo michezo 72 katika misimu minne na kuhusika kwenye mabao 47, akifunga 30 na kutoa asisti 17.


Pia amefanikiwa 
kuitumikia timu ya taifa ya DR Congo katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika
kwa wachezaji wanaocheza 
ligi ya ndani (CHAN) iliyofanyika mwaka huu nchini Cameroon ambapo
alifunga mabao mawili na 
kutoa asisti moja

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
Next articleBOSI YANGA ASIMULIA NAMNA AMBAVYO WALIMPA MKATABA SURE BOY