METACHA MNATA ATAJWA KUIBUKIA YANGA

MLINDA mlango namba moja wa Klabu ya Polisi Tanzania, Metacha Mnata rasmi amevunja mkataba na aliyekuwa meneja wake Jemedari Said.

Hili limekuja wakati huu ambapo Metacha anazungumzwa kuhitajika na Yanga ambao watakosa huduma ya kipa wao namba moja raia wa Mali Diarra ambaye anakwenda kujiunga na Timu yake ya Taifa katika michuano ya AFCON.

Kwa sasa Yanga wanatajwa kusaka kipa ambaye ataungana na Johore kwenye majukumu ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na mechi nyingine za ushindani kwa kuwa Ramadhan Kabwili anatajwa kwamba anaweza kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Jana Desemba 24 usajili wa kwanza wa Yanga ulitangazwa ambapo ni kiungo Sure Boy kutoka Azam FC.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa bado wana mpango wa kufanya usajili hivyo taarifa zitatolewa hivi karibuni.

Ikumbukwe kwamba Mnata aliibuka Polisi Tanzania baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya kikosi hicho msimu uliopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mnata ameandika namna hii:”Nachukua nafasi hii kukushukuru kwa muda wote na kuwa pmoja katika maisha yangu na wakati umefika wa kukushukuru sana kila la kheli katika ufanisi wako Jemedar Said,”.