Home Sports PABLO HANA TATIZO NA PASCAL WAWA

PABLO HANA TATIZO NA PASCAL WAWA

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kilichotokea kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC ni kutoelewana na mwamuzi.

Jana Pablo akiwa benchi alionekana kumzuia Pascal Wawa asiweze kuingia kuendelea kutimiza majukumu yake.

Kwenye mchezo huo ubao wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ulisoma KMC 1-4 Simba na kuiwafanya mabingwa hao watetezi kusepa na pointi tatu.

Pablo amesema:”Suala hili halikuhitaji ufafanuzi lakini ni jambo ambalo limetokea katika mchezo wetu hasa katika upande wa mabadiliko.

“Jambo lililotokea naweza kusema ni kushindwa kuwa na mawasiliano mazuri na mwamuzi katika suala la mabadiliko lakini mambo mengine yanakwenda sawa.

“Sina tatizo na mchezaji Wawa kwa kuwa ni mchezaji mzuri na anatimiza majukumu yake,” amesema Pablo.

Previous articleMETACHA MNATA ATAJWA KUIBUKIA YANGA
Next articleBURUDANI YA SOKA KUENDELEA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU!