
HUYU HAPA ATAJWA KUWA MBADALA WA DIARRA YANGA
INASEMEKANA Yanga imemfuata rasmi kipa namba moja wa Mtibwa Sugar, Abuutwalib Mshery kwa ajili ya kumsajili katika dirisha dogo msimu huu kuwa mbadala sahihi wa Djigui Diarra. Wakati Yanga ikimfuata Mshery, ina mpango wa kuachana na kipa wake, Ramadhani Kabwili ambaye msimu huu amekuwa hana nafasi. Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa, Yanga imepanga kumsajili kipa mzawa mwenye uwezo na uzoefu wa ligi atakayekuwa mbadala wa Diarra anayetarajiwa…