ATLETICO Madrid imefanikiwa kufuzu kwenda hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Porto huku staa wake Luis Suarez akiwa haamini anachokiona na kumwaga machozi baada ya kuumia na kutolewa uwanjani.
Atletico ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao hayo 3-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Do Dragao,Porto.
Suarez alianza kikosi cha kwanza alitolewa dakika ya 13 na akaenda benchi huku akimwaga machozi.
Timu hiyo ilikuwa kundi B la maajabu ambalo lilikuwa na Liverpool, Porto, AC Milan na Atletico wenyewe na zilizofuzu ni Liverpool na Atletico watakwenda 16 bora na Porto wao watakwenda Europa.