Home Sports AZAM YAFUNGUKIA USAJILI WA SURE BOY YANGA

AZAM YAFUNGUKIA USAJILI WA SURE BOY YANGA

UONGOZI wa Azam FC umetoa kauli kuhusu tetesi za Kiungo wa klabu hiyo Salum Abubakar ‘Suare Boy’ kuhusishwa na mpango wa kuwa mbioni kusajiliwa ndani ya kikosi cha Yanga.

‘Sure Boy’ anayetumikia adhabu ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana huko Azam Complex, anatajwa kuwa kwenye mpango wa kusajiliwa na Yanga wakati wa dirisha dogo la usajili, ambalo rasmi litafunguliwa Desemba 15.

Akizungumzia jambo hilo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC, Zakaria Thabiti ‘Zaka Zakazi’ amesema taarifa za mchezaji huyo kuwa mbioni kusajiliwa Yanga wanaziona kwenye mitandao ya kijamii, lakini hazijawafikia rasmi mezani kwao.

Amesema Azam FC haina hiyana yoyote katika suala la kumuachia mchezaji anayehitajiwa na klabu nyingine, lakini akasisitiza kufuatwa kwa taratibu za uhamisho ambazo zinatambulika duniani kote.

“Sisi hatumzuii mchezaji yeyote kusajiliwa na timu nyingine, kikubwa timu husika inahitajika kufuata taratibu za usajili,” amesema Zaka Zakazi.

Sure Boy alisimamishwa na Azam FC mwanzoni mwa msimu huu kwa utovu wa nidhamu, sanjari na wachezaji Mudathir Yahya na Aggrey Morris.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE CHAMPIONI IJUMAA
Next articleASINGEKUWA RONALDO,MESSI SALAH ANGEKUWA STAA DUNIANI