Home International ASINGEKUWA RONALDO,MESSI SALAH ANGEKUWA STAA DUNIANI

ASINGEKUWA RONALDO,MESSI SALAH ANGEKUWA STAA DUNIANI

MOHAMMED Salah baada ya kufunga goli 20 na kutoa asisti za goli tisa katika michuano yote, Pat Nevin amesema kama dunia isingekuwa kwenye nyakati za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi basi Salah angekuwa staa kwa sasa.

Bao moja ambalo Salah alilifunga kwenye mechi ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan kwenye ushindi wa 2-1 mtanange uliopigwa Uwanja wa San Siro Italia umemfanya kuwa mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga angalau goli 20 kwa misimu mitano mfululizo. Mchezaji pekee mwenye rekodi yakufunga misimu sita alikuwa Ian Rush.

“Bila uwepo wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo tungemuona vipi Mohamed Salah kwa sasa, bila shaka angekuwa staa mkubwa mno? Alijaribu kuuliza Pat Nevin.

Kwa upande wake kocha wa Celtic Neil Lennon amesema Mohammed Salah ni mchezaji bora anayemkaribia kabisa Lionel Messi kwa miaka kadhaa iliyopita.

Salah, 29, ni mchezaji wa zamani wa Chelsea na AS Roma maeneo ambayo hakuwa na kiwango kizuri kama ambacho kwa sasa anakionesha Liverpool.

Previous articleAZAM YAFUNGUKIA USAJILI WA SURE BOY YANGA
Next articleHUYU HAPA ATAJWA KUWA MBADALA WA DIARRA YANGA