Home Sports HUYU HAPA ATAJWA KUWA MBADALA WA DIARRA YANGA

HUYU HAPA ATAJWA KUWA MBADALA WA DIARRA YANGA

INASEMEKANA Yanga imemfuata rasmi kipa namba moja wa Mtibwa Sugar, Abuutwalib Mshery kwa ajili ya kumsajili katika dirisha dogo msimu huu kuwa mbadala sahihi wa Djigui Diarra.


Wakati Yanga ikimfuata Mshery, 
ina mpango wa kuachana na kipa wake, Ramadhani Kabwili ambaye msimu huu amekuwa hana nafasi.


Mmoja wa mabosi wa Yanga, 
ameliambia Spoti Xtra kuwa, Yanga imepanga kumsajili kipa mzawa mwenye uwezo na uzoefu wa ligi atakayekuwa mbadala wa Diarra anayetarajiwa kwenda kucheza AFCON mwakani akiwa na kikosi cha Mali.


Bosi huyo alisema wakati Diarra 
akiwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Mali, anatakiwa awepo kipa mwingine atakayesaidiana na Erick Johora.


Aliongeza kuwa, kati ya makipa 
wanaotajwa kuichezea Yanga katika usajili wa dirisha dogo yupo kipa tegemeo wa Mtibwa Sugar, Mshery ambaye wameanza naye mazungumzo.


“Wapo makipa wengi 
wanaotajwa kuja kusajiliwa na Yanga katika dirisha dogo na kati ya hao yupo wa Mtibwa ambaye ni Mshery.


“Uongozi upo katika hatua za 
mwisho za kukamilisha usajili wake baada ya kuwafuata viongozi wa Mtibwa kwa ajili ya mazungumzo.


“Hivyo dili hilo muda wowote 
litakamilika baada ya viongozi wa pande mbili watakapofikia sehemu nzuri ya kuvunja mkataba na Mtibwa,” alisema bosi huyo.


Mjumbe wa Kamati ya 
Mashindano wa Yanga, Injinia Hersi Said, hivi karibuni aliliambia Spoti Xtra kuwa:
“Masuala yote ya usajili 
tumemuachia kocha wetu Nabi (Nasreddine), tayari tumepokea mapendekezo kadhaa ya usajili kutoka kwake katika usajili wa dirisha dogo ambayo tunayafanyia kazi.”

Previous articleASINGEKUWA RONALDO,MESSI SALAH ANGEKUWA STAA DUNIANI
Next articleMKWANJA WAWEKWA WA KUTOSHA KWA SIMBA KISA YANGA