Home International MKATABA WA SALAH KLOPP ANENA

MKATABA WA SALAH KLOPP ANENA

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool ameweka wazi kuwa suala la mkataba wa mshambuliaji wake nyota Mohamed Salah raia wa Misri linahitaji muda.

Kwa sasa kumekuwa na mvutano mkubwa kuhusu mkataba wa Salah ambaye amebakisha miezi 19 huku akitaka dau nono na mabosi hao wamekuwa wakionekana kuzingua kwa muda.

Nyota huyo hivi karibuni akiwa nchini Misri aliweka wazi kuwa wanaopaswa kumaliza suala hilo ni Liverpool wenyewe na yeye atakuwa na furaha ikiwa atabaki ndani ya Anfield.

Klopp amesema:”Tunazungumzia suala la mchezaji aina ya Salah kuongeza mkataba siyo suala la kama kukutana kwenye kahawa jioni na kufikia makubaliano.

“Mo amezungumza mambo machache na mimi ninaweza kusema kuwa yaliyobaki sio ya kuweka hadharani lakini Mo yupo sawa na mimi nipo sawa na mambo haya yanahitaji muda,”

Previous articleMWAMUZI AGOMA KUCHEZESHA DABI,NDANI YA CHAMPIONI JUMATANO
Next articleSIMBA WATUA DAR, HESABU NI DHIDI YA YANGA KWA MKAPA