BOCCO AYEYUSHA DAKIKA KIBAO BILA KUFUNGA

JOHN Bocco nahodha wa Simba anakibarua kizito cha kutetea kiatu chake cha ufungaji bora huku akiwa ametumia jumla ya dakika 387 uwanjani bila kufunga wala kutoa pasi ya bao.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2020/21 Bocco alisepa na kiatu cha ufungaji bora baada ya kufunga mabao 16 na alitoa pasi mbili za mabao.

Kwa sasa ndani ya Simba kinara wa utupiaji ni Meddie Kagere mwenye mabao manne na pasi moja ya bao aliyompa mshikaji wake Kibu Dennis kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting.

Kocha Msaidizi wa Simba, Hitimana Thiery aliliambia Spoti Xtra kuwa washambuliaji wa timu hiyo wamekuwa wakikosa utulivu katika kumalizia nafasi zinazotengenezwa jambo linalowafanya washindwe kufunga.

“Kwenye mechi zetu kuna wachezaji ambao wanashindwa kutumia nafasi ambazo wanazipata hilo tumeliona na tunalifanyia kazi ili waweze kufunga,” alisema Hitimana.