SIMBA V YANGA MATOKEO MSIBEBE MFUKONI

  PRESHA kubwa kwa sasa ni kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Desemba 11, ambao ni wa watani wa jadi wanakutana kusaka pointi tatu muhimu.

  Mashabiki wanahitaji kuona matokeo chanya kwa timu zao na mshindi ni yule ambaye atafanya maandalizi mazuri kwa wakati huu. Ipo wazi kwamba utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

  Jambo la msingi kuelekea kwenye mchezo huo kwa sasa kwa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) ni kuangalia namna gani mashabiki wanaweza kuwa salama pamoja na wageni ambao watajitokeza.

  Uzuri ni kwamba kila mmoja anaweza kupata ushindi na ile ambayo itashindwa kujiandaa haitaweza kupata ushindi kwani kila kitu ni maandalizi.

  Kikubwa ambacho kinahitajika kwa mashabiki ambao watajitokeza Uwanja wa Mkapa kuacha kubeba matokeo uwanjani na kuendelea kufanya maandalizi yao kwa hesabu ili kupata pointi tatu.

  Kila timu inapaswa kupambana ili kupata kile ambacho kinastahili kwa kuwa jambo la msingi ni kila mchezaji kutimiza jukumu lake uwanjani.

  Mashabiki ambao watabeba matokeo mfukoni huwa inakuwa ngumu kwao kuamini kile ambacho watakiona baada ya dk 90 kukamilika hivyo jambo la msingi ni kujiandaa kusubiri matokeo uwanjani.

  Imani yangu ni kwamba kila timu imefanya maandalizi mazuri kwa mechi ambazo wamecheza na ambacho kinafanyika kwa sasa ni kusubiri muda ufike ili kazi iweze kuonekana uwanjani.

  Ukweli ni kwamba kila mmoja anapenda kupata ushindi lakini ushindi haupatikani ikiwa kutakuwa hakuna maandalizi mazuri kila timu inaweza kushinda lakini ni lazima ijiaandae.

  Kwa upande wa mashabiki ambao watajitokeza kazi yao iwe moja kushangilia bila kuleta vurugu hilo pia halifai kwa soka letu la sasa ambalo lina ushindani mkubwa.

  Kila timu ipambane kwa wakati huu kupata matokeo huku Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) likitazama namna gani inaweza kuwa katika mpangilio mzuri kwa namna ya kuwafanya mashabiki wafurahi mpira bla bugudha.

  Kwenye maisha ya soka kila kitu kinawezekana na mambo kubadilika ni mara moja tu hivyo ikiwa walipata nafasi wakashindwa kuzitumia basi wasiwashushie lawama wachezaji.

  Jambo la msingi kwa waamuzi ambao wamepewa jukumu la kusimamia mechi hiyo ni lazima wafuate sheria 17 za soka ili kwenda sawa.

  Imekuwa kawaida kwa mechi hizi zenye presha waamuzi kufanya maamuzi ambayo ni hasara kwa timu moja hilo lisipewa nafasi.

  Kwa upande wa wachezaji nao wamekuwa wakitumia nguvu kusaka ushindi hilo nalo lisipewa nafasi nguvu kubwa pia ni hasara kwani itaigharimu timu kwa mchezaji kuweza kuonyeshwa kadi nyekundu ama ile ya njano.

  Mipango ni sasa na maandalizi mazuri ni lazima ili kupata ushindi baada ya dakika 90 kila kitu kinawezekana.

  Previous articleBOSI SIMBA ABAINISHA KUWA USHINDI UPO
  Next articleYANGA:MOTO HAUZIMI