Home Sports BOSI SIMBA ABAINISHA KUWA USHINDI UPO

BOSI SIMBA ABAINISHA KUWA USHINDI UPO

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’, amesema kuwa Yanga ni watoto wadogo kwa Simba na timu yao ipo tayari kuchukua alama tatu, Desemba 11.

Try Again alisema wao wanauchukulia mchezo wao na Yanga kama michezo mingine wanayocheza kwenye ligi na kwamba suala la kupata ushindi kwenye mchezo huo ni zaidi ya asilimia 90.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Try Again alisema kila kitu kimeshakamilika kabla hata hawajasafiri kwenda Zambia na kilichobaki ni kwa upande wa wachezaji kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja.

“Yanga kwetu ni timu ya kawaida, hatuna hofu nao hata kidogo, mchezo huo wa dabi tunaona kama mechi nyingine za ligi ambazo huwa tunacheza na timu kutoka nje na Dar es Salaam,” .

Tayari kikosi cha Simba kimerejea Dar, Desemba 7 ambapo kilikuwa nchini Zambia kwenye mchezo dhidi ya Red Arrows ambao ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho.

Simba inakumbuka kwaba Septemba 25 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ilipoteza kwa kuungwa bao 1-0 na Yanga na mtupiaji alikuwa ni Fiston Mayele.

 

Previous articleJINA LA AUSSEMS LATAJWA NAMUNGO
Next articleSIMBA V YANGA MATOKEO MSIBEBE MFUKONI