


BREAKING: MECHI YA KAGERA SUGAR V SIMBA IMEAHIRISHWA
RASMI mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba umeahirishwa. Mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa leo Desemba 18, Uwanja wa Kaitaba na maandalizi yalikuwa yamekamilika kwa timu zote mbili. Jana kwenye kikao na Waandishi wa Habari, Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba alibainisha kuwa karibu robo tatu ya wachezaji wa timu…

WAAMUZI MSIJIKAUSHE,KUTOCHAGULIWA AFCON NI TATIZO LENU KUBWA
IMETOKA orodha ya waamuzi waliopata nafasi ya kuchezesha michuano ya Afcon lakini kwa Tanzania hakuna ambaye amechaguliwa. Waamuzi waliotaganzwa kuchezesha michuano hiyo, wapo kutoka karibu kila nchi hata zile za jirani kama Uganda na Rwanda lakini Tanzania haina nafasi. Nasema Tanzania haina nafasi baada ya kutopata nafasi hata ya mwamuzi mmoja aliyeteuliwa katika hatua hiyo…

NYOTA HAWA KUTOLEWA KWA MKOPO YANGA
IKIWA kwa sasa dirisha dogo la usajili limefunguliwa nyota watatu wa Yanga wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kutolewa kwa mkopo ili waweze kupata changamoto mpya katika timu nyingine kutokana na kukosa nafasi kikosi cha kwanza. Nyota hao ni pamoja na Abdalah Haji, beki huyu wa kati mzawa kwenye mechi nane za Yanga amecheza mechi moja…

WACHEZAJI SIMBA WAKUMBWA NA HOMA
WACHEZAJI wa Simba ambao leo wana kazi ya kusaka ushindi mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara wanakabiliwa na homa pamoja na mafua. Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Simba, mzawa Seleman Matola ameweka wazi kuwa wameweza kufika salama Kagera kwa ajili ya mchezo huo na wapo tayari lakini kuna baadhi ya…

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumamosi.

BARAZA:TUPO TAYARI KUIKABILI SIMBA
FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaoatarajiwa kuchezwa kesho, Desemba 18. Itakuwa ni Uwanja wa Kaitaba ambapo tayari timu ya Simba imeshawasili Bukoba kwa ajili ya maandalizi ya mwisho wa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa….

UWANJA WA SIMBA KUGHARIMU BILIONI 30,KAMPENI YAZINDULIWA
UONGOZI wa Klabu ya Simba leo Desemba 17,2021 umezindua kampeni maalumu kwa ajili ya mashabiki,wanachama na wadau kuweza kuchanga fedha kwa ajili ya gharama za ujenzi wa kisasa. Uwanja huo wa Mo Simba Arena gharama zake ambazo zinatarajiwa kutumika ni zaidi ya Bilioni 30 na wameweka wazi kwamba utakuwa ni mchakato endelevu na matumizi ya…

MIAKA MINNE YA GAZETI LA SPOTI XTRA
Desemba 17, 2017, Gazeti la Spoti Xtra liliingia mtaani kwa mara ya kwanza. Tangu hapo, hadi leo Desemba 17, 2021, limetimiza miaka minne likiendelea kufanya vizuri na kuteka wasomaji wengi ambao wamekuwa wadau wetu wakubwa. Unaouona hapo, ni ukurasa wa mbele wa nakala ya kwanza ya Gazeti la Spoti Xtra. Ubora wa timu ya Spoti…

NYOTA WA SIMBA NA YANGA WAANZA KAZI GEITA GOLD
KOCHA Mkuu wa Geita Gold Fredy Felix Minziro, leo Desemba 17 ameanza kuwatumia wachezaji wake wapya katika kikosi chake kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu. Maingizo hayo mapya yamekipiga ndani ya timu kongwe Simba na Yanga ni pamoja na beki wa kazi chafu, Juma Nyoso ambaye aliwahi kucheza Simba, Mbeya City na Kagera Sugar…

UBORA WA SIMBA WATAJWA KUWA UPO KWENYE VIUNGO
ABDALAH Mohamed, ‘Bares’ Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa ubora wa Simba upo kwenye viungo jambo ambalo liliwafanya washindwe kupata matokeo mazuri walipokutana nao Uwanja wa Mkapa. Simba Desemba 14 iliweza kushinda bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya tatu ambapo bao la ushindi lilifungwa na Kibu…

MASTAA WANNE WA YANGA KUIKOSA TANZANIA PRISONS
IKIWA leo timu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddne Nabi inaelekea Sumbawanga kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons itawakosa mastaa wake wanne kikosi cha kwanza. Leo Desemba 17 kikosi kitapita Mbeya kabla ya kuibukia Sumbawanga ambapo kitakuwa na mchezo dhidi ya Prisons, Desemba 19. Ni Yacouba Songne ambaye ni majeruhi…

RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO DESEMBA 17
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea kwa sasa ambapo leo Desemba 17 kuna mechi ambazo zitachezwa. Geita Gold itashuka Uwanja wa Nyankumbu kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting. Mbeya Kwanza itakuwa na kibarua Uwanja wa Sokoine dhidi ya Namungo FC. Dodoma Jiji v Polisi Tanzania, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

MASTAA YANGA WAPIGWA MKWARA NA MTUNISSIA
NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kwamba hakuna mchezaji mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga kwa kuwa Yanga ni kubwa kuliko yoyote. Kocha huyo raia wa Tunissia ameongeza kuwa kuhusu kuanza kikosi cha kwanza kwa wachezaji wake itategemea na namna hali itakavyokuwa kutokana na mchezo husika na haina maana kwamba kufunga mabao ni…

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Ijumaa

TIMU MBALIMBALI KUENDELEA KUTIFUANA WIKIENDI HII, NANI NI NANI?
Bundesliga, Serie A na EPL kunogesha wikiendi yako. Wakati baadhi ya vilabu vya EPL vikihaha na maambukizi ya Omicron Variant, nchi zingine mambo yanaendelea kama kawaida, kwa kuzingatia tahadhari dhidi ya COVID-19. Wikiendi inakwenda namna hii; Bayern Munichen watakuwa pale Allianz Stadium kuwaalika Wolfsburg Ijumaa hii. Huu ni mchezo ambao unazikutanisha timu mbili zenye…

WAZIRI NDUMBARO ASHINDA MASHINDANO YA GOFU
WAZIRI wa Maliasili, Dkt Damasi Ndumbaro ameibuka mshindi wa mashindano ya Gofu ya Wabunge ya Afrika Mashariki kwa ushindi wa jumla akiwakilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waziri Ndumbaro amepata jumla ya pointi 73 katika ushindi wa jumla zilizofanya aweze kuibuka kidedea. Ndumbaro amesema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa kwa kuwa kila mshiriki alikuwa…