MIAKA MINNE YA GAZETI LA SPOTI XTRA

Desemba 17, 2017, Gazeti la Spoti Xtra liliingia mtaani kwa mara ya kwanza. Tangu hapo, hadi leo Desemba 17, 2021, limetimiza miaka minne likiendelea kufanya vizuri na kuteka wasomaji wengi ambao wamekuwa wadau wetu wakubwa.

Unaouona hapo, ni ukurasa wa mbele wa nakala ya kwanza ya Gazeti la Spoti Xtra.

Ubora wa timu ya Spoti Xtra kuanzia kwa mhariri mtendaji, wahariri, waandishi, wapiga picha, wasanifu kurasa na wafanyakazi wote wa Global Publishers, umelifanya gazeti hili kuwa namba moja kila linapoingia mtaani Jumanne, Alhamisi na Jumapili.

Tunachukua nafasi hii kuwashukuru wote wanaoendelea kuwa nasi.

Tukiwa tunauanza ukurasa mpya wa kuhesabu miaka mingine ya mapambano, tunaahidi mambo mazuri zaidi yanakuja. Baki na sisi.

SPOTI XTRA NI UHONDO TU