BARAZA:TUPO TAYARI KUIKABILI SIMBA

FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaoatarajiwa kuchezwa kesho, Desemba 18. Itakuwa ni Uwanja wa Kaitaba ambapo tayari timu ya Simba imeshawasili Bukoba kwa ajili ya maandalizi ya mwisho wa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa….

Read More

MIAKA MINNE YA GAZETI LA SPOTI XTRA

Desemba 17, 2017, Gazeti la Spoti Xtra liliingia mtaani kwa mara ya kwanza. Tangu hapo, hadi leo Desemba 17, 2021, limetimiza miaka minne likiendelea kufanya vizuri na kuteka wasomaji wengi ambao wamekuwa wadau wetu wakubwa. Unaouona hapo, ni ukurasa wa mbele wa nakala ya kwanza ya Gazeti la Spoti Xtra. Ubora wa timu ya Spoti…

Read More

NYOTA WA SIMBA NA YANGA WAANZA KAZI GEITA GOLD

KOCHA Mkuu wa Geita Gold  Fredy Felix Minziro, leo Desemba 17 ameanza kuwatumia wachezaji wake wapya katika kikosi chake kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu. Maingizo hayo mapya yamekipiga ndani ya timu kongwe Simba na Yanga ni pamoja na beki wa kazi chafu, Juma Nyoso ambaye aliwahi kucheza Simba, Mbeya City na Kagera Sugar…

Read More

UBORA WA SIMBA WATAJWA KUWA UPO KWENYE VIUNGO

ABDALAH Mohamed, ‘Bares’ Kocha Mkuu wa JKT Tanzania amesema kuwa ubora wa Simba upo kwenye viungo jambo ambalo liliwafanya washindwe kupata matokeo mazuri walipokutana nao Uwanja wa Mkapa. Simba Desemba 14 iliweza kushinda bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya tatu ambapo bao la ushindi lilifungwa na Kibu…

Read More

MASTAA WANNE WA YANGA KUIKOSA TANZANIA PRISONS

IKIWA leo timu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddne Nabi inaelekea Sumbawanga kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons itawakosa mastaa wake wanne kikosi cha kwanza. Leo Desemba 17 kikosi kitapita Mbeya kabla ya kuibukia Sumbawanga ambapo kitakuwa na mchezo dhidi ya Prisons, Desemba 19. Ni Yacouba Songne ambaye ni majeruhi…

Read More

RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO DESEMBA 17

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea kwa sasa ambapo leo Desemba 17 kuna mechi ambazo zitachezwa. Geita Gold itashuka Uwanja wa Nyankumbu kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting. Mbeya Kwanza itakuwa na kibarua Uwanja wa Sokoine dhidi ya Namungo FC. Dodoma Jiji v Polisi Tanzania, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

Read More

MASTAA YANGA WAPIGWA MKWARA NA MTUNISSIA

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kwamba hakuna mchezaji mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga kwa kuwa Yanga ni kubwa kuliko yoyote. Kocha huyo raia wa Tunissia ameongeza kuwa kuhusu kuanza kikosi cha kwanza kwa wachezaji wake itategemea na namna hali itakavyokuwa kutokana na mchezo husika na haina maana kwamba kufunga mabao ni…

Read More