KOCHA Mkuu wa Geita Gold Fredy Felix Minziro, leo Desemba 17 ameanza kuwatumia wachezaji wake wapya katika kikosi chake kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu.
Maingizo hayo mapya yamekipiga ndani ya timu kongwe Simba na Yanga ni pamoja na beki wa kazi chafu, Juma Nyoso ambaye aliwahi kucheza Simba, Mbeya City na Kagera Sugar pamoja mshambuliaji Ditram Nchimbi ambaye amewahi kucheza Yanga, Azam FC na Njombe Mji.
Leo Mizinro anakiongoza kikosi cha Geita Gold kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Sooting ambapo Nyoso ameanza kikosi cha kwanza na Nchimbi yeye anasugua benchi kwanza.
Nchimbi msimu wa 2021/22 hakuwa na nafasi ndani ya Yanga na alicheza mchezo mmoja pekee katika ile nane huku akitumia dakika 13 chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.