Home Sports BARAZA:TUPO TAYARI KUIKABILI SIMBA

BARAZA:TUPO TAYARI KUIKABILI SIMBA

FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unaoatarajiwa kuchezwa kesho, Desemba 18.

Itakuwa ni Uwanja wa Kaitaba ambapo tayari timu ya Simba imeshawasili Bukoba kwa ajili ya maandalizi ya mwisho wa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Baraza amabeinisha kwamba wachezaji wake wengi bado hawajawa imara sana kutokana na uchovu wa mchezo dhidi ya Azam FC ambao ulikamilika kwa sare ya bila kufungana lakini haina maana kwamba hawapo tayari kwa ajili ya mchezo wao.

“Tumetoka kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC haukuwa mwepesi na naona kwamba wachezaji wako na uchovu na pia wengine baadhi wanasumbuliwa na majeraha lakini ripoti ya daktrai itanipa muongozo juu ya hali zao.

“Tunatarajia mchezo utakuwa mgumu lakini kwa kuwa tupo nyumbani basi tutapambana kupata pointi tatu, tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tutafanya vizuri,” amesema.

 

Previous articleUWANJA WA SIMBA KUGHARIMU BILIONI 30,KAMPENI YAZINDULIWA
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI