MASTAA WANNE WA YANGA KUIKOSA TANZANIA PRISONS

IKIWA leo timu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddne Nabi inaelekea Sumbawanga kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons itawakosa mastaa wake wanne kikosi cha kwanza.

Leo Desemba 17 kikosi kitapita Mbeya kabla ya kuibukia Sumbawanga ambapo kitakuwa na mchezo dhidi ya Prisons, Desemba 19.

Ni Yacouba Songne ambaye ni majeruhi wa muda mrefu anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa msimu mzima, Fiston Mayele huyu aliumia mguu wa kulia lakini kwa sasa anaendelea vizuri.

Pia yupo beki wa kupanda na kushuka mzawa Kibwana Shomari ambaye anatarajiwa kuwa nje kwa muda wa wiki nne pamoja na mshambuliaji Athuman ambaye alipata maumivu ya mguu.

Mayele amekuwa na pacha nzuri na mshikaji wake Feisal Salum ambapo wote wametupia mabao matatu ndani ya ligi kwa msimu wa 2021/22.

Hivyo Feisal atakuwa kwenye majukumu na pacha ya nyota wengine ndani ya kikosi hicho kinachoongoza ligi na pointi 20 baada ya kucheza jumla ya mechi nane.