BREAKING: MECHI YA KAGERA SUGAR V SIMBA IMEAHIRISHWA

RASMI mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba umeahirishwa.

 

Mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa leo Desemba 18, Uwanja wa Kaitaba na maandalizi yalikuwa yamekamilika kwa timu zote mbili.

Jana kwenye kikao na Waandishi wa Habari, Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba alibainisha kuwa karibu robo tatu ya wachezaji wa timu ya Simba walikuwa wanasumbuliwa na homa pamoja na mafua.

“Asilimia kubwa wachezaji wetu wanasumbuliwa na mafua na homa ni karibia robo tatu ya wachezaji hii nadhani inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa,”