Home Sports WAZIRI NDUMBARO ASHINDA MASHINDANO YA GOFU

WAZIRI NDUMBARO ASHINDA MASHINDANO YA GOFU

WAZIRI wa Maliasili, Dkt Damasi Ndumbaro ameibuka mshindi wa mashindano ya Gofu ya Wabunge ya Afrika Mashariki kwa ushindi wa jumla akiwakilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Ndumbaro amepata jumla ya pointi 73 katika ushindi wa jumla zilizofanya aweze kuibuka kidedea.

Ndumbaro amesema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa kwa kuwa kila mshiriki alikuwa anahitaji ushindi lakini mazoezi ya mara kwa mara ni siri ya ushindi.

“Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa na kila mmoja wetu alijipanga kuwa mshindi. Siri ya ushindi wangu ni mazoezi ya mara kwa mara na uzoefu,”.

Mashindano ya Gofu ya Mabunge Afrika Mashariki yamefanyika katika Uwanja wa Kill Golf uliopo USA River.

Upande wa Wabunge Wanawake, Neema Mgaya, (Tanzania) yeye amepata jumla pointi 48 zilizompa ushindi upande huo, ilieleza taarifa hiyo.

Previous articleVIDEO: MERIDIAN YAJA NA SOKA LA MTAANI
Next articleTIMU MBALIMBALI KUENDELEA KUTIFUANA WIKIENDI HII, NANI NI NANI?