
SIMBA INA MATUMAINI NA KUTWAA UBINGWA
MTENDAJI wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez, amesisitiza kuwa ishu ya nani atakuwa bingwa wa ligi kuu msimu huu, ipo wazi kwamba Simba ndiyo watachukua tena kombe. Barbara amefunguka kuwa, msimu huu wanakutana na changamoto nyingi ambazo anaamini zinatengenezwa makusudi ili kuwakwamisha Simba, ila wanataka kuonyesha watu kuwa Simba ni timu kubwa haswaambayo ikitaka jambo lake lazima lifanikiwe. Akizungumzia ugumu wa ligi msimu huu, Barbara alikiri kuwepo kwa ushindani zaidi…