Home Sports SIMBA INA MATUMAINI NA KUTWAA UBINGWA

SIMBA INA MATUMAINI NA KUTWAA UBINGWA

MTENDAJI wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez, amesisitiza kuwa ishu ya nani atakuwa bingwa wa ligi kuu msimu huu, ipo wazi kwamba Simba ndiyo watachukua tena kombe.

Barbara amefunguka kuwa, msimu huu wanakutana na changamoto nyingi ambazo anaamini zinatengenezwa makusudi ili kuwakwamisha Simba, ila wanataka kuonyesha watu kuwa Simba ni timu kubwa haswa
ambayo ikitaka jambo lake lazima 
lifanikiwe.

Akizungumzia ugumu wa ligi msimu huu, Barbara alikiri kuwepo kwa ushindani zaidi ya msimu uliopita, ila hiyo kwao haiwezi kuwa kikwazo cha kutaka kuweka rekodi ya kuchukua ubingwa kwa mara ya tano mfululizo.

Licha ya upinzani na ugumu wanaokutana nao kwenye kila kona ya uwanja na nje pia.

“Suala la Simba kuwa bingwa msimu huu lipo wazi kabisa na halina mjadala, Simba ndiyo itachukua ubingwa. Tunakutana na ugumu na changamoto kubwa lakini hatuwezi kushindwa kabisa.

“Tutapambana hadi mwisho kuwapa furaha wapenzi na mashabiki wetu wa Simba, tunataka kuwaonyesha kuwa Simba ni timu kubwa ambayo inaweza kupambana kwenye mazingira yote yanayokuja mbele yetu,” alisema.

Leo Januari 26,2022 Simba inatarajiwa kumenyaa na Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Kaitaba.

Previous articleUBABE KWENYE KOMBE LA SHIRIKISHO UWEKWE KANDO
Next articleMTIBWA SUGAR:TUNA BAJETI YA MIAKA 40