Home Sports MTIBWA SUGAR:TUNA BAJETI YA MIAKA 40

MTIBWA SUGAR:TUNA BAJETI YA MIAKA 40

THOBIAS Kifaru,Ofisa Habari mwenye uwezo mkubwa wa kuzungumza na nidhamu kubwa katika kazi yake ameweka wazi kwamba timu hiyo ina bajeti ya kujiendesha kwa muda wa miaka 40.

Mtibwa Sugar kwa sasa inatumia Uwanja wa Manungu ambao ulikuwa umefungiwa kwa muda ili kuweza kufanyiwa maboresho na kwa sasa tayari umeruhisiwa kutumika.

Mchezo uliopita Mtibwa Sugar iliwakaribisha Simba kwenye mchezo wa ligi na ulitoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana.

Kifaru amesema:”Hatutegemei mapato ya mlangoni ili kuweza kuendesha timu yetu kwa kuwa tuna bajeti ya miaka 40 kwa ajili ya kuweza kuendesha timu yetu hii.

“Sisi Uwanja wa Manungu ni mzuri na bora tumeufanyia maboresho na umepitishwa kwamba unafaa kutumika kwenye mechi za ligi.

“Kikubwa ni kuweza kuwapa mashabiki burudani na mechi zetu zitachezwa hapa bila mashaka yoyote yale tupo tayari na tutazidi kupambana,” amesema.

Previous articleSIMBA INA MATUMAINI NA KUTWAA UBINGWA
Next articleBOCCO,KAGERE WAANZIA BENCHI DHIDI YA KAGERA SUGAR