Aston Villa yatwaa ubingwa wa Europa League kwa kishindo dhidi ya Freiburg

Aston Villa wameandika historia mpya baada ya kutwaa ubingwa wa UEFA Europa 2026 kufuatia ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya SC Freiburg katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye dimba la Beşiktaş Park.

Kocha Unai Emery ameendelea kuthibitisha ubora wake kwenye michuano hiyo baada ya kuweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa taji la Europa League akiwa na vilabu vitatu tofauti; Sevilla, Villarreal na Aston Villa. Hili ni taji lake la tano kwenye mashindano hayo, rekodi inayomfanya kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Europa League.

Mabao ya Aston Villa yalifungwa na:
⚽ 41’ Youri Tielemans
⚽ 45+3’ Emiliano Buendía
⚽ 58’ Morgan Rogers