Sheria Mpya, Matukio Tata Michuano ya Dunia 2026

Michuano ya Dunia ya FIFA 2026 limeanza kwa kuvunja rekodi kadhaa za kihistoria. Siku sita tu baada ya mechi ya ufunguzi kati ya Mexico na Afrika Kusini uwanjani Estadio Azteca (waliohudhuria 80,824), mashindano yaliweka rekodi mpya ya idadi kubwa zaidi ya mashabiki kuhudhuria siku moja watu 281,223 katika mechi nne za Ufaransa dhidi ya Senegal, Iraq dhidi ya Norway, Argentina dhidi ya Algeria na Austria dhidi ya Jordan, wakivunja rekodi ya awali ya 277,070 iliyowekwa mwaka 1994.

Kufikia tarehe 25 Juni, jumla ya mashabiki waliohudhuria mashindano ilivuka rekodi ya wote wa aina yake ya milioni 3.5 iliyowekwa 1994, wakati wa mechi ya Ecuador dhidi ya Ujerumani katika uwanja wa New York New Jersey.

Rekodi hizo za mahudhurio zimeambatana na sheria mpya za IFAB zilizoanza kutumika mashindano haya. Miongoni mwazo ni sekunde kumi za lazima kwa mchezaji anayetoka uwanjani wakati wa mabadilishano, count down ya sekunde tano kwa mirushano ya kando na migongo ya lango, mapumziko ya dakika tatu ya kunywa maji kila nusu ya mchezo, na VAR iliyopanuliwa kuweza kupitia upya kona zisizo sahihi na kadi nyekundu za kadi mbili za njano.

Vilevile, mpira rasmi wa Adidas Trionda unaobeba vitambuzi vya ndani umewezesha teknolojia ya “off-side” ya nusu-otomatiki kufanya kazi kwa usahihi mkubwa zaidi kuliko mashindano yaliyopita. Hata hivyo, si rekodi zote zilizohusiana na michezo yenyewe.

Uwanja wa Los Angeles Stadium ulizua mjadala mkali baada ya mechi ya ufunguzi ya Marekani dhidi ya Paraguay, ambapo licha ya kutangazwa rasmi kuwa viti vyote vimejaa (mashabiki 70,492), picha za televisheni zilionyesha viti tupu maeneo ya VIP, hali iliyochochea malalamiko kuhusu bei kubwa za tiketi.

Uwanja wa Guadalajara nao ulijitokeza kwenye mijadala kama hiyo wakati wa mechi ya Korea Kusini dhidi ya Czechia. Kwa upande mwingine, uwanja mdogo zaidi wa BMO Field jijini Toronto uliandikisha mahudhurio ya asilimia 99.8 ya uwezo wake wakati wa mechi ya Ghana dhidi ya Panama, ushahidi kwamba si viwanja vyote vikubwa vilivyoshuhudia rekodi.

Kwenye upande wa maamuzi ya kiuchezaji, rekodi za VAR zimekuwa na utata mwingi zaidi kuliko idadi ya mashabiki. Mabao ya Iran dhidi ya Misri na Brazil dhidi ya Scotland yalifutwa hatua ya makundi, huku Folarin Balogun wa Marekani akipewa kadi nyekundu dhidi ya Bosnia kabla FIFA haijaibatilisha.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Hivi karibuni zaidi, bao la Misri lililofutwa dakika za mwisho dhidi ya Argentina uwanjani Atlanta liliongeza tena hisia za ukosefu wa uwiano katika matumizi ya teknolojia hiyo, licha ya lengo lake la awali kuwa ni kuongeza usahihi.

Kwa jumla, rekodi za viwanjani za michuano ya  dunia 2026 zinaonesha picha mbili tofauti: upande mmoja ni mafanikio makubwa ya kihistoria ya mahudhurio na miundombinu, na upande mwingine ni changamoto za kudumu za bei za tiketi, uwazi wa VAR, na uwiano wa maamuzi ya waamuzi.

Mashindano yanapoendelea kuelekea hatua za mwisho, itakuwa muhimu kuona kama FIFA itaweza kudumisha rekodi hizi huku ikiziba mianya ya utata iliyojitokeza tangu mechi ya kwanza.