Home International COMOROS BADO WANAISHI KWENYE AKILI ZA WATU AFCON

COMOROS BADO WANAISHI KWENYE AKILI ZA WATU AFCON

LICHA ya timu ya taifa ya Comoros kutolewa kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Cameroon katika hatua ya 16 bora ya Afcon 2021 timu hiyo bado imekaa kwenye mioyo ya watu kutokana na upambanaji wao bila kuchoka.

Comoros ambao waliinyoosha Ghana katika mchezo wa mwisho wa kundi C na kupita wakiwa ni best losers juzi walionyesha kiwango bora dhidi ya Cameroon.

Wachezaji hao walipambana licha ya kwamba walicheza pungufu tangu dakika ya 16 tena walicheza bila ya uwepo wa kipa wao namba moja na namba mbili pamoja na yule namba tatu hivyo ngoma ilibidi langoni akae beki wa kushoto Chaker Alhadhur ambaye aliweza kuwashangaza watu.

Ali Ahamada na Moyadh Ousseni walikuwa na Corona huku Salim Ben Boina akiwa na jeraha la bega na kocha wao Amir Abdou ambaye naye ana Corona.

Kwenye mchezo wenyewe ilikuwa ni mambo ya Kiafrika zaidi kwa kuwa dakika ya sita tu Nadjim Abdou alitolewa kwa kadi nyekundu na kufanya mambo yazidi kuwa magumu kwao zaidi.

Cameroon wapo nyumbani walitangulia kupata ushindi kupitia kwa Karl Toko Ekambi na Vincent Aboubakar huku Youssouf M’Changama akiifungia bao pekee na nusura waweke mzani sawa dakika za mwisho.

Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO
Next articleUBABE KWENYE KOMBE LA SHIRIKISHO UWEKWE KANDO