YANGA WAMPA TANO NABI
NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amefunguka kuwa kwa sasa nyota wa kikosi hicho wanafurahia zaidi mfumo wa soka la pasi nyingi, ambao unafundishwa na kocha mkuu Nasrredine Nabi, kulinganisha na utamaduni wao wa awali wa kutumia mipira mirefu. Tangu msimu huu umeanza kocha Nabi anaonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibadilisha Yanga ambayo sasa inacheza mpira wa pasi nyingi, tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wakitumia mipira mirefu. …