>

HASSAN DILUNGA APEWA TUZO YAKE HUKO MSIMBAZI

HASSAN Dilunga kiungo wa wa Wekundu wa Msimbazi, Simba amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Oktoba inayodhaminiwa na Emirates Aluminium ACP kwa kuwashinda Sadio Kanoute na Rally Bwalya aliokuwa nao fainali.

 

Kwa mwezi Oktoba, Dilunga amekuwa ni chaguo la kwanza kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na alianza pia kwenye mchezo walionyooshwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneg Galaxy huu ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Licha ya kusepana tuzo hiyo hakuwa na bahati ya kuyeyusha dakika zote 90 kwenye mechi ambazo alianza msimu huu wa 2021/22.

Katika viungo hao watatu walioingia fainali ni mmoja tu alifanikiwa kutupia alikuwa ni Bwalya ambaye alifunga kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy pamoja na ule mchezo wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwe kwamba kipa namba moja Aishi Manula hakuwepo ambapo alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kaimu Kocha, Hitimana Thiery.