OFISA wa Yanga, Haji Manara amechagua kikosi bora kwa msimu wa 2021/22 baada ya timu zote kucheza jumla ya mechi tano.
Uzuri ni kwamba haya ni maoni ya Manara yeye mwenyewe lakini ajabu ni kwamba kwenye kikosi hicho hakuna mchezaji mmoja kutoka kikosi cha Simba ambacho msimu uliopita wa 2020/21 alikuwa anataja kuwa ni kikosi bora kwa kuwa alikuwa Ofisa Habari wa Simba.
Manara amesema kuwa suala la uchambuzi alianza muda mrefu na hiki ni kikosi chake bora baada ya mechi tano.
Hiki hapa ni kikosi cha Manara ambaye amekipanga namna hii:-
Diarra Djigua wa Yanga huyu ni kipa.
Djuma Shaban wa Yanga
Dickson Job wa Yanga
Bakari Nondo wa Yanga
Kibwana Shomari wa Yanga
Jesu Moloko wa Yanga
Yanick Bangala wa Yanga
Khalid Aucho wa Yanga
Feisal Salum wa Yanga
Fiston Mayele wa Yanga
Vitalis Mayanga wa Polisi Tanzania
toa maoni yako kuhusu kikosi hicho.