Home Uncategorized VARANE KUZIKOSA MAN CITY, CHELSEA, ARSENAL

VARANE KUZIKOSA MAN CITY, CHELSEA, ARSENAL

Beki wa kati Raphael Varane anatarajiwa kuukosa mchezo wa Manchester derby kwenye Uwanja wa Old Trafford, wikiendi hii kutokana na kuwa majeruhi.

Varane alipata maumivu ya nyama za paja alipokuwa akiitumikia Manchester United ikicheza dhidi ya Atalanta katika Champions League, Jumanne ya wiki hii na imeelezwa kuwa atakuwa nje kwa mwezi mmoja.

Hiyo inamaanisha Varate atakosa mechi dhidi ya Manchester City, Watford, Villarreal, Chelsea na Arsenal pindi atakapokuwa nje ya uwanja.

Hiyo ni habari mbaya kwa Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer ambaye amekuwa na safu mbovu ya ulinzi.
.

Previous articleWASHINDI WA BONUS WA JACKPOT YA SPORTPESA HAWA HAPA
Next articleDAKIKA 450 ZA JASHO JINGI SIMBA