YANGA WAMPA TANO NABI

NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amefunguka kuwa kwa sasa nyota wa kikosi hicho wanafurahia zaidi mfumo wa soka la pasi nyingi, ambao unafundishwa na kocha mkuu Nasrredine Nabi, kulinganisha na utamaduni wao wa awali wa kutumia mipira mirefu.

 

Tangu msimu huu umeanza kocha Nabi anaonekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibadilisha Yanga ambayo sasa inacheza mpira wa pasi nyingi, tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wakitumia mipira mirefu.

 

Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara mpaka sasa wakiwa na asilimia 100 ya ushindi ambapo
wamefanikiwa kujikusanyia pointi 15, 
katika michezo mitano waliyocheza mpaka sasa.


Akizungumza na Championi Ijumaa, 
Mwamnyeto alisema: “Ni jambo zuri kuona tumeuanza msimu huu kwa matokeo mazuri ambapo mpaka sasa tunaongoza msimamo, najua kila mmoja anaona mabadiliko makubwa ya kiuchezaji jambo ambalo kama wachezaji tunalifurahia zaidi.


“Hatukuwa na muda mrefu wa 
maandalizi ya kabla ya msimu, lakini kocha amefanya kazi kubwa
kutengeneza muunganiko wa kikosi 
ambao unaleta matokeo mazuri na soka la kuvutia.