USAJILI UZINGATIE RIPOTI YA BENCHI LA UFUNDI
HEKAHEKA za usajili wa dirisha dogo ndani ya Ligi Kuu Bara zimeanza huku timu nyingi zikianza mikakati ya kuviboresha vikosi vyao kuelekea mzunguko wa pili ili ziweze kufanya vizuri kwenye ligi na michuano mingine ambayo watashiriki. Kipindi hiki timu zinapaswa kuwa makini katika kuhakikisha wachezaji ambao watasajiliwa waendane na mahitaji ya benchi la ufundi…