>

RASMI: SURE BOY ATAMBULISHWA YANGA

BREAKING: RASMI Kiungo Salum Aboubakhari ametambulishwa Yanga akiwa mchezaji huru.

Nyota huyo alikuwa anakipiga ndani ya Azam FC ambapo mkataba wake ulikuwa unatarajiwa kumeguka msimu huu lakini aliomba kuvunja mkataba.

Hiyo ilitokana na matatizo ya kinidhamu ambapo ilipelekea akasimamishwa kwa muda usiojulikana na hata walipoambiwa warudi kambini Sure Boy hakuwa tayari kurudi aliomba kuvunjiwa mkataba wake.

Anajiunga na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kwa dili la miaka miwili.