UWANJA wa Ali Hassan Mwinyi dakika 45 zimekamilika kwa timu mbili kuonyeshana ubabe wa kusaka pointi tatu muhimu.
Ubao kwa sasa unasoma KMC 1-2 Simba hivyo timu zote zinakwenda mapumziko zikiwa zimepata bao na Simba inaongoza.
Mohamed Hussein alianza kupachika bao la kuongoza ilikuwa dakika ya 10 kisha dakika ya 12 Onyango Joash alipachika bao la pili kwa Simba.
KMC walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Abdul Hillary dakika ya 40 kwa shuti kali lililomshinda kipa namba moja wa Simba,Aishi Manula.