Home Sports DAKIKA 90, KMC 1-4 SIMBA

DAKIKA 90, KMC 1-4 SIMBA

SIMBA watakula Christmas wakiwa na pointi zao tatu kibindoni baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya KMC.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa na mashabiki wengi walijitokeza Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kushuhudia mchezo huo.

Simba waliweza kupachika mabao yao kupitia kwa Mohamed Hussein dk 10,Joash Onyango dk 13 na Kibu Dennis alipachika mabao mawili ilikuwa dakika ya 47 na 57 walitupia mabao kwa Simba.

Abdul Hillary alifunga kwa KMC dk 41 na kufanya KMC iweze kupoteza pointi tatu ikiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 21 huku KMC ikibaki kuwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi 10 na Simba imecheza mechi 9.

Previous articleDAKIKA 45: KMC 1-2 SIMBA
Next articleBREAKING:VIDEO:SURE BOY RASMI NI MALI YA YANGA