MSUVA APANDIWA DAU NA YANGA ,SIMBA
WAKATI dirisha dogo la usajili hapa nchini likifungwa usiku wa kuamkia leo Jumapili, kulikuwa na mchuano mkali kwa timu za Simba na Yanga kwa ajili ya kupata saini ya kiungo mshambuliaji wa Wydad Casablanca ya Morocco, Mtanzania, Simon Msuva. Msuva aliondoka Yanga, Julai 29, 2017, akiwa ameisaidia kuvuna mataji matatu mfululizo ya Ligi Kuu Bara na kutua Difaa El Jadida ya Morocco, kisha Novemba 10, 2020, akajiunga na Wydad. Habari zimeeleza kwamba,…