Home Sports RASMI CHAMA NI MALI YA SIMBA

RASMI CHAMA NI MALI YA SIMBA

RASMI sasa Clatous Chama ni mali ya Simba akitokea Klabu ya RS Berkane ambapo alikuwa huko akikipiga.

Aliibuka msimu wa 2021/22 akitokea Simba lakini kwenye mkataba wake mpya kulikuwa na suala la kurejea ndani ya timu hiyo ikiwa kutakuwa na makubaliano ya pande zote mbili.

Unakuwa ni usajili wa kwanza kutangazwa rasmi na Simba katika dirisha dogo baada ya tetesi kuwa nyingi kuhusu Chama.

Kwa mujibu wa Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa nyota huyo atawasaidia katika mechi za ligi.

“Chama ni mwenzetu na tutakuwa naye ambapo atatusaidia katika mechi za ligi pamoja na mashindano mengine,”.

Previous articleMASHINDANO YA AFCON, KANDANDA LA EPL NA SERIE A ZOTE KUTOA BURUDANI
Next articleYANGA YAMSAJILI BEKI KISIKI WA KMKM ??????? ?????