Home Sports YANGA YAMALIZANA NA JEMBE HILI LA KAZI

YANGA YAMALIZANA NA JEMBE HILI LA KAZI

KLABU ya Yanga imemtambulisha rasmi nyota Ibrahim Bacca kuwa ni njano na kijani kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo msimu wa 2021/22.

Nyota huyo wa zamani wa KMKM,Malindi na Taifa Jang’ombe sasa atakuwa ndani ya Ligi Kuu Bara chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Anaungana na Salim Aboubakhari, ‘Sure Boy’,Dennis Nkane,Aboutwalib Mshery ambao ni nyota wapya waliosajiliwa na Yanga.

Ni katika usajili wa dirisha dogo ambao unatarajiwa kufungwa rasmi kesho Januari 15.

Kwa mujibu wa Nabi amesema kuwa anahitaji wachezaji wenye uwezo ambao atafanya nao kazi katika kikosi chake.

Previous articleGEITA GOLD KAMILI KUIVAA DODOMA JIJI
Next articleMASHINDANO YA AFCON, KANDANDA LA EPL NA SERIE A ZOTE KUTOA BURUDANI