KIKOSI cha Geita Gold kimeshatia timu makao makuu ya nchi Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Januari 15 Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Geita Gold ni miongoni mwa timu ambazo zimepanda ligi msimu huu na imeweza kufanya usajili wa nyota wakongwe katika usajili wa dirisha dogo.
Miongoni mwa nyota ambao imewasajili ni pamoja na Juma Nyosso, Kelvin Yondani na Ditram Nchimbi ambao tayari wameshaanza kazi kwenye mechi za ligi.