Home Sports YANGA YAIPIGIA HESABU COASTAL UNION

YANGA YAIPIGIA HESABU COASTAL UNION

OFISA Habari wa Yanga, Haji Manara ameweka wazi kuwa mchezo wao wa kesho dhidi ya Coastal Union waanaamini utakuwa mgumu lakini wanahitaji pointi tatu kwenye mchezo huo wa ligi.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi inaongoza ligi ina pointi 29, Januari 16 inatarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union iliyo nafasi ya nne na pointi 17 kibindoni.

Manara amesema kwamba wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kupata pointi tatu kwa kuwa ili kufikia malengo ambayo wanahitaji ni lazima washinde kwenye mechi ngumu.

“Tupo tayari na tunataka pointi tatu kwenye mchezo wetu dhidi ya Coastal Union. Tunakumbuka kwamba msimu uliopita mchezo wetu tulipokutana nao Uwanja wa Mkwakwani tulifungwa hivy hatuchukulii kwamba utakuwa mchezo rahisi.

“Mashabiki wetu wa hapa Tanga na maeneo yote ambao watakuja hapa kutushangilia wawe na imani kwamba tunakwenda kufanya vizuri, tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunachohitaji ni pointi tatu,”.

Msimu uliopita Yanga iliweza kupoteza mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani jambo linalowafanya waende kwa tahadhari kubwa.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo Tanga ni pamoja na Dennis Nkane. Yassin Mustapha,Mukoko Tonombe,Jesus Moloko.

Previous articleKMC KAMILI KUIVAA TANZANIA PRISONS
Next articleMATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA, YAPO HAPA