Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo Jumamosi, Januari 15, 2022 limetangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2021.
Matokeo hayo yametangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde ambapo pia, baraza hilo limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji wa kitaifa ya darasa la nne na kidato cha pili 2021.
Akitangaza matokeo hayo, Dkt. Msonde amesema watahiniwa wa Shule 422,388 (87.30%) kati ya Watahiniwa 483,820 wamefaulu Mitihani yao ongezeko la ufaulu ni 1.46% ikilinganishwa na mwaka 2020.
Bonyeza kila kiungio hapa chini kuona matokeo husika;
MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2021
MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2021
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2021