
KIUNGO SERGIO GOMEZ NI MALI YA CITY
SERGIO Gomez ambaye ni kiungo amesaini dili la miaka minne kuweza kuitumikia Klabu ya Manchester City. City ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England wameinasa saini ya nyota huyo ili aweze kupata changamoto mpya ndani ya Ligi Kuu England. Nyota huyo mwenye miaka 21 amesajiliwa kwa dau la pauni milioni 11 akitokea Klabu ya Anderlecht…