Home Sports MUDA WA MAANDALIZI UMEFIKA KWA SASA ILI KAZI IENDELEE

MUDA WA MAANDALIZI UMEFIKA KWA SASA ILI KAZI IENDELEE

MUDA wa kazi umefika kwa kuwa kulikuwa na ule wa maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23 ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

Kufika tamati wa maandalizi ya msimu uliopita inamaana kwamba sasa tunakwenda kuanza jambo lingine na  kutokana na namna ambavyo timu zimejipanga litakuwa ni jambo la maana kweli.

Tayari ratiba imeshatolewa hivyo inamaanisha kwamba kila timu imeshajua itaanza na nani na zipo timu ambazo zimeshafunga safari kuwafuata wapinzani wao.

Nina amini kwamba ligi ya msimu ujao ambao ni mpya itakuwa ya kipekee na yenye ushindani mkubwa hivyo kila mmoja lazima aweke mipango vizuri.

Kwa namna ambavyo timu itakuwa imeweza kufanya maandalizi yake itakuwa kwenye namna yake ya kupata matokeo hivyo ni suala la kusubiri na kuona itakuaje tena msimu mpya.

Tusisahau kwamba kwa sasa pia ni wakati mzuri wa kuweza kuanza kukamilisha mipango kazi kwa msimu mpya wa 2022/23.

Kuna timu ambazo ziliweza kucheza hatua ya mtoano na kupata nafasi ya kubaki kwenye ligi na nyingine zilipanda kutoka Championship huku zingine zikishuka hata msimu ujao pia itakuwa hivyo.

Ipo wazi kwamba maisha ya kwenye Championship ni magumu mwanzo mwisho na ushindani ni mkubwa kila timu inatimiza majukumu yake kupata ushindi hivyo kila mmoja aweze kuliweka akilini hilo.

Katika usajili na maandalizi yote yanahitaji umakini mkubwa kwa kuwa hakuna ambaye hapendi kupata yale ambayo wanastahili hasa kwa kujipanga upya.

Wachezaji kazi yao ni moja kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ili waweze kupata kile wanachokistahili,kikubwa ni mipango kazi na ushirikiano.

Ni wakati mzuri wa kujipanga tena na timu kuangalia yale ambayo waliweza kuyafanya msimu uliopita na kukwama kupata ushindi hasa kwenye mechi zijazo.

Kila mmoja anapenda kuona matokeo mazuri na huwa hayatokei kwa wepesi hasa kutokana na ukweli kwamba ni muda halisi wa kujipanga na kufanya kweli.

Benchi la ufundi kwa sasa linakazi kubwa kuweza kujenga upya vikosi kazi ili kufanya kazi kweli kwenye ushindani wa msimu ujao inawezekana na kila kitu ni maandalizi.

Tunaona kwamba wapo ambao wanafanya usajili muda huu na wengine wameshamaliza hilo linapaswa kuendelea pale inapohitajika mpaka itakapofika kikomo dirisha likifungwa.

Kwa kila timu nina amini kwamba imena yale mapungufu ambayo yalikuwa kwenye kikosi hivyo usajili utazingatia yale makosa na kusajili wachezaji wazuri zaidi.

Zipo timu ambazo zinakwenda kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye mechi za kimataifa hapo napo ni wakati wa kufanya maandalizi kwa wakati.

Ipo wazi kwamba mashindano ya kimataifa yanahitaji maandalizi mazuri ili kuweza kupata matokeo chanya kwenye kila mechi.

Hakuna ambaye anapenda kuona kwamba kwenye mashindano ya kimataifa kwa mara nyingine tena kuona kila mmoja anashindwa kusonga mbele.

Muhimu ni maandalizi mazuri na kila mmoja kwa sasa anawajibu wa kufanya kazi yale makosa ambayo aliyaona kwa wakati ule alipoweza kushiriki kimataifa.

Ukweli ni kwamba kwenye mashindano ya kimataifa ni njia ambayo inaweza kuwapa nguvu wachezaji na kuwapeleka kwenye soko la kimataifa.

Kupata nafasi nne ni jambo kubwa na linapaswa kutunzwa kwa vitendo kwa timu ambazo zinakwenda kushiriki mashindano ya kimataifa.

Kila timu imeweza kutambua wapinzani wao hivyo pia ni wakati wa kufanya maandalizi mazuri kwa mechi za kimataifa ambazo zinahitaji akili na nguvu kubwa pia.

Wachezaji watakaopata nafasi kwenye mashindano ya kimataifa jukumu lao ni moja kusaka ushindi kwa hali na mali hii itawapa nafasi ya kuweza kufikia malengo yao binafsi pamoja na timu.

Previous articleVIDEO:NABI:DABI ILIKUWA YAKIMBINU,TULIWAPA KUJIAMINI KUCHEZA
Next articleRATIBA YA MECHI ZA LEO LIGI KUU BARA