Home Sports RATIBA YA MECHI ZA LEO LIGI KUU BARA

RATIBA YA MECHI ZA LEO LIGI KUU BARA

ILE burudani ambayo ilikuwa imekosekana kwa muda sasa inarejea kwa kasi ambapo ni leo Agosti 15,viwanja viwili vitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu.

Ihefu FC ya Mbeya itawakaribisha Ruvu Shooting huku Namungo FC wao watamenyana na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

 Ihefu inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila imerejea kwenye ligi kwa mara nyingine baada ya kushuka msimu wa 2020/21.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting,Masau Bwire amesema kuwa wanatambua msimu utakuwa na ushindani ila wapo tayari kusaka ushindi.

“Msimu mpya unaanza nasi tunakuja kwa tofauti kabisa,makosa ambayo tulifanya msimu uliopita benchi la ufundi limefanyia kazi hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

Thobias Kifaru,Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa usajili ambao wamefanya utawapa matokeo chanya.

Previous articleMUDA WA MAANDALIZI UMEFIKA KWA SASA ILI KAZI IENDELEE
Next articleTEN HAG AAMBIWA ALIKOSEA KUPANGA KIKOSI