Home Sports MAYELE CHINI YA ULINZI

MAYELE CHINI YA ULINZI

KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania,Joslin Sharif amesema kuwa amezungumza na mabeki wake kuhakikisha kwamba hawafanyi makosa mbele ya Yanga leo kwa kumlinda mshambuliaji Fiston Mayele asije kuwaadhibu pamoja na wachezaji wengine.

Mayele ni mshambuliaji namba moja ndani ya Yanga ambapo alikamilisha msimu wa 2021/22 akiwa ametupia mabao 16 na pasi nne za mabao leo anakwenda kukabiliana na Polisi Tanzania.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,Arusha majira ya saa 10:00 jioni.

Kocha huyo ambaye amechukua mikoba ya Malale Hamsini amesema:”Tunamshukuru Mungu kikosi kipo salama na morali ni kubwa kuelekea kwenye mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Yanga ambao unatarajiwa kuwa mgumu na ushindani mkubwa.

“Tunatambua umuhimu wa mchezo wetu na tumeona wapinzani wana kikosi kizuri lakini hata sisi tumesajili wachezaji wazuri, Mayele ni mchezaji mzuri na anajua kufunga lakini ana miguu miwili kama ambavyo wachezaji wetu wanayo hivyo tutacheza naye kwa tahadhari,” amesema.

Msafara wa wachezaji 25 wa Yanga upo Arusha ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa leo ambao ni wa kwanza kwa msimu wa 2022/23.

Previous articleMAKI KWENYE KIBARUA KINGINE
Next articleKAPOMBE:MASHABIKI WAJITOKEZE KUTUPA SAPOTI