Home Sports KAPOMBE:MASHABIKI WAJITOKEZE KUTUPA SAPOTI

KAPOMBE:MASHABIKI WAJITOKEZE KUTUPA SAPOTI

SHOMARI Kapombe, nahodha msaidizi wa Simba amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kesho kushuhudia mchezo wao dhidi ya Geita Gold.

Simba inaingia uwanjani kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ikiwa imetoka kutunguliwa mabao 2-1 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Beki huyo ambaye hakucheza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Yanga ameweka wazi kwamba anatambua mashabiki wanahitaji furaha na ushindi hivyo wajitokeze kwa wingi.

“Tunaanza msimu mpya yale ambayo yalitokea msimu ule tunakwenda kuyafanyia kazi na tunaamini kwamba benchi la ufundi limeweza kufanyia kazi na kutupa mbinu ambazo tutazitumia kwenye mechi zetu.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwa kuwa wao ni muhimu na wamekuwa nasi kwenye mechi nyingi ambazo tulicheza nasi tutajitahidi kufanya vizuri ili kuweza kushinda mechi zetu,” amesema.

Previous articleMAYELE CHINI YA ULINZI
Next articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA POLISI TANZANIA