Klabu zinazoshiriki Premier League zimeombwa kuunga mkono hoja iliyowasilishwa na Klabu ya Wolverhampton Wanderers inayopendekeza azimio la kupiga Kura ya kufuta Matumizi ya ‘VAR’ kuanzia Msimu ujao
–
Pendekezo hilo ambalo linadaiwa kupingwa na Bodi ya Ligi Kuu linatarajiwa kusikilizwa Juni 6, 2024 ambapo imeelezwa Bodi inatambua haki ya Wolves kutoa pendekezo hilo, lakini inadhani kufutwa kwa #VAR kunaweza kusababisha maamuzi mengi yasiyo sahihi
–
Aidha, baadhi ya Maafisa wa EPL wanadai pendekezo hilo litaathiri Ubora wa Ligi, pia kwa mujibu wa takwimu za Msimu huu zinaonesha kiwango cha maamuzi sahihi ya Uwanjani kimeongezeka kutoka 82% hadi 96 kupitia VAR
Official Website