Home Sports MBWANA SAMATTA NI KRC GENK

MBWANA SAMATTA NI KRC GENK

AGOSTI 16,2022 Klabu ya KRC Genk imemtambulisha Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Mbwana Samatta kuwa ni nyota wao mpya.

Samatta anarejea kwenye klabu hiyo baada ya kupata changamoto mpya Januari 2020 na kuhamia Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England.

Samatta amejiunga na Genk akitokea Klabu ya Fenerbahçe kwa mkataba wa mwaka mmoja hadi mwisho wa msimu, ambapo miamba hao wa Ubelgiji watakuwa na chaguo la kumsajili moja kwa moja.

Msimu uliopita, Samatta alikuwa ndani ya Klabu ya Royal Antwerp ya Ubelgiji kwa mkopo na aliweza kutimiza majukumu yake na timu hiyo iliweza kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Europa League msimu huu.

Samatta anarudi Genk akiwa na kumbukumbu ya kucheza michezo 191, mabao 76, pasi za magoli 20 kwenye mashindano yote, kiatu cha dhahabu pamoja na ubingwa wa ligi kuu Jupiler Pro League (2018/19).

Kila la Kheri Samatta kwenye hatua nyingine kwa wakati mwingine.

Previous articleSAUTI:MZUNGU WA SIMBA ANA KAZI NZITO YA KUFANYA
Next articleHII HAPA RATIBA YA LIGI LEO NA MATOKEO